.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Aprili 2014

KIJANA WA MIAKA 16 ASAFIRI KWA KUTUMIA TAIRI LA NDEGE HUKO MAREKANI

 Kijana mwenye umri wa miaka 16, amefanikiwa kusafiri kutoka San Jose, California hadi Maui, Hawaii kwa kujificha katika moja ya matairi ya ndege ya shirika la ndege la Hawaiian Airline namba 45 bila kupata matatizo yeyote pamoja na hali ya hewa na kusafiri kwa saa tano angani, jambo ambalo wengi wameliona kama miujiza. 

Msemaji wa FBI, Tom Simon ameliambia shirika la habari la AP kuwa, walimkamata kijana huyo baada ya kumuona akikatiza katika uwanja wa Maui bila kitambulisho. 

Simon amesema kuwa, picha za kamera katika uwanja wa San Jose California zinamuonyesha kijana huyo kutoka Santa Clara akiruka uzio wa uwanja na kwenda katika ndege hiyo jumapili asubuhi. 

Inasemekana kijana huyo ambaye hakutajwa jina lake, aliondoka nyumbani kwao baada ya kutokea mvutano, na ndege ilipotua katika uwanja wa ndege wa Maui, alishuka salama kutoka katika tairi alilokuwa amejificha na kuanza kukatiza uwanjani hapo kabla ya kukamatwa
                                                        Akipelekwa Hospitali kuangaliwa afya yake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni