.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Aprili 2014

WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA ASTAAFU SIASA ,JK AMPONGEZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa viongozi wengine wakuu wa serikali chama cha Mapinduzi CCM, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (kushoto) katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania mara mbili katika awamu mbili tofauti, Mzee Cleopa David Msuya (wa kwanza kulia kwa Rais) ambaye amestaafu rasmi siasa baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 33
Katibu wa CCM, wilaya ya Mwanga, akisoma historia fupi ya Mzee Msuya kabla na baada ya kujiunga na siasa.
Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM wilaya ya Mwanga, Joseph Thadayo akitoa salamu za marafiki na wasomi waishio nje ya Mwanga, ikiwemo salamu za Mwanasiasa maarufu na mdhamini wa CCM, Mzee Peter Kisumo ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na mzee Msuya katika Siasa 
Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.
 Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.

Kwa hisani ya Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.





Hakuna maoni :

Chapisha Maoni