.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Julai 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAANDALIA FUTARI WANANCHI WA PEMBA


Baadhi ya waumini wa Nini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba wakifutari pamoja hapo ikulu ya Wete futari iliyoandaliwa na
Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akawakilishwa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ,h. Mohd Aboud Mohd kati kati akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi kulia yake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee
Mberwa Hamad Mberwa wakijumuika na wananachi wa mikoa miwili ya Pemba kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Kikwete mara baada ya futari ya pamoja kwa wananchi wa mikoa miwili ya Pemba.

Balozi Seif akiwaaga na baadhi ya wananchi wa mikoa miwili ya pemba waliohudhuria futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete hapo Ikulu ya Wete Pemba.

Balozi Seif akibadilishana mawazo na mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Dr. Mrisho Kikwete hapo wete Pemba.
                                                                  
                                                         Picha na Hassan Issa wa – OMPR ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao kama inavyoagiza wakati wote.

Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili ya Wananchi wa Miko miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya Ikulu ya Serikali ya Muungano yaliyopo Mjini Wete
Pemba.

Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa waislam hupatikana katika mjumuisho wa makundi ya ibada akiyataja kuwa ni pamoja na madrsasa, sala pamoja na mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futari ya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao. 

Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa Zanzibar .

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jkaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada hiyo.

Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia hufanywa ba baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni atika kujipatia futari.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni