.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Agosti 2014

LIGI KUU UINGEREZA MAMBO BADO MAGUMU KWA MANCHESTER UNITED, WALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA BURNLEY

 Ugumu wa kupata mabao umeendelea kuikumba Manchester United katika ligi kuu ya Uingereza baada ya leo kwa mara nyingine ikijikuta ikitoka uwanjani bila kuzoa point tatu muhimu kwao kutokana na kubanwa vilivyo na Burnley na kulazimishwa sare ya kutofunga katika mchezo wa mapema wa ligi kuu Uingereza uliomalizika punde.
 Ikicheza na nyota wake karibu wote akiwemo Wyane Rooney, Juan Matta, Robin van Persie pamoja na Angel Di Maria ambaye huu ni mchezo wake wa kwanza toka asajiliwe kutoka Real Madrid ya Hispania, Mashetani hao wekundu walishindwa kabisa kutikisa nyavu za wenyeji wao Burnley waliohakikisha lango lao wana lilinda muda wote. 

Hii ni mechi ya tatu mfululizo katika ligi kuu kwa Man United kuendelea kufanya vibaya, mchezo wa kwanza walifungwa 2-1 na Swansea, wakalazimishwa sare ya baoa 1-1 na Sunderland na leo wametoka vichwa chini kwa mara nyingine.
                  Kocha wa Manchester United Louis van Gaal akiufuatilia mchezo huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni