.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Septemba 2014

DC BUSEGA AHAGIZA VYOMBO HUSIKA KUFUATILIA HARAKA KUBAKWA KWA MWALIMU WA SEKONDARI.


                          Mkuu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Bw Paul Mzindakaya
Na.Shushu Joel ,Busega,simiyu

Mkuu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu Bw, Paul .C. Mzindakaya ameviagiza vyombo husika kufuatilia mara moja suala la kubakwa kwa mwalimu wa shule ya sekondari Kishamapanda iliyoko katika kata ya Mwamanyili wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hayo leo mara baada ya kuwasili katika masomo yake nje ya nchi. 

Amesema kuwa hapa nchini kuna matukio mengi sana yanayotokea lakini katika wilayani yake tangu awe mkuu wa wilaya hajawai kusikia suala la unyama kama huo, hivyo ameviagiza vyombo husika kulifanyia haraka iwezekanavyo suala hili la kumdhalilisha mwalimu huyo na hata kumfanya kukosa amani ya kuishi katika wilaya yake.


" Suala hili limenifanya kuonekana mnyonge sana na mwenye kukosa amani kabisa na ninawataka watu hao waliofanya tukio hili wapatikane kwa haraka sana ili sheria iweze kuchukua mkondo wake na pia aliongeza kuwa ushaidi ukiwa tayari basi hukumu ya kesi hiyo iwe ni ya kuigwa kwa wale wenye tabia za unyama wa namna hiyo" alisema.

Aidha Mzindakaya aliwata wananchi wa Nassa gineri kuweza kutoa ushilikiano wa kutosha kwa polisi ili waeze kufanya kazi yao kwa urahisi na ufanisi ya kuwabaini watu hao waliofanya ukatili huo wilayani hapa na ni jambo la fedhea kubwa sana katika wilaya yetu ya upendo ,ukalimu na ushilikiano na hata kuifanya kuwa wilaya bora za mkoa wa simiyu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni