.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 1 Septemba 2014

VIJANA WASHAURIWA KUJIAJIARI KATIKA SEKTA YA SANAA


Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.


Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.


Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini – WHVUM

Vijana kutoka Afrika ya Mashariki wameshauriwa kujikita katika sekta ya sanaa kwani ni fani ambayo inatoa nafasi kubwa ya ajira kwa vijana hivyo kuondokana na tatizo la ajira katika nchi za Afrika Mashariki.

Rai hiyo imetolewa na Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara wakati wa ziara ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) hivi karibuni katika Wilaya ya Bagamoyo.

Dk. Mukangara amesema kuwa TaSUBa ni kituo cha Maarifa kinachotoa masomo ya sanaa za maonyesho yaani ngoma za jadi na michezo ya kuigiza na sanaa ya ufundi wa uchoraji na ufinyangaji Afrika ya Mashariki hivyo ni vyema kwa vijana kujiunga na chuo hicho ili waweze kupata taaluma na kuweza kujiajiri wenyewe.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe. Spika wa bunge la EALA Bi. Magreth Zziwa amesema kuwa masuala ya Sanaa na Utamaduni ni muhimu sana katika jamii zetu kwani Utamaduni hujenga umoja, utambulisha jamii husika na kuthamini utajiri wa mila na desturi za waafrika.

Mhe. Zziwa amesema kuwa Bunge la Afrika Mashariki limejumuisha vituo mbalimbali vya Maarifa vyenye weledi Afrika ya Mashariki na katika vituo hivyo TaSUBa ni moja ya kituo cha Maarifa chenye rasilimali watu, wingi wa ubunifu na mitaala iliyopangika kwani sifa mojawapo ya kituo cha Maarifa kuwa na weledi ilikua ni kituo kuwa na mpango mkakati ambapo TaSUBa wanao.

Aidha Mhe. Zziwa ameitaka TaSUBa kupenya nchi zote za Afrika ya Mashariki na kuwa na brandi ya Kiswahili kitakachotumika Afrika ya Mashariki pamoja na brandi ya kiutamaduni na kisanaa itakayohusisha nchi hizo kwa kutangaza shughuli mbalimbali za kiutamaduni vikiwemo vyakula vya Afrika ya Mashariki, mavazi na aina ya muziki wetu.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa kutoka TaSUBa Bw. Michael Kadinde amesema kuwa TaSUBa imeandaa mitaala mipya mbalimbali kwa sasa itakayotumika kwa ajili ya wanafunzi watakao jiunga na Taasisi hiyo kutoka Afrika ya Mashariki.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ni taasisi yaSerikali chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ilianzishwa kwa sharia ya wakala wa serikali Na. 30 ya mwaka 1997 inayotoa mafunzo, utafiti na ushauri katika masuala ya Sanaa na Utamaduni nchini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni