Waandamaji makumi kwa maelfu
wamekusanyika na kuandamana kwa siku ya pili nchini Burkina Faso
kaika mji Mkuu wa Ouagadougou, wakimtaka rais Blaise Compaore
kujiuzuru.
Viongozi wa upinzani jana usiku
walitumia mitandao ya kijamii kuitisha maandamano mapya, wakionyesha
kuchukizwa na rais Compaore ambaye alikaririwa baada ya maandamano ya
siku ya kwanza kuwa ataendelea kuwa madarakani kwa kipindi cha mwaka
mmoja akiongoza serikali ya mpito.
Katika tamko hilo rais Compaore pia
alikubali kutogombea tena baada ya waandamanaji kuchoma majengo ya
serikali.
Kuundwa kwa serikali ya mpito
kulitangazwa na mkuu wa majeshi nchini humo Jenerali Honore Traore
ambaye amesema atashirikisha vyama vyate vya siasa na pia alitangazwa
kuvunjwa kwa bunge la nchi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni