.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 1 Novemba 2014

NHC WATATHMINI UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MIRADI YAKE


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza jambo katika semina hiyo.

Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma, Itandula Gambalagi akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo, Kongwa Dodoma kwenye semina ya mameneja na wakurugenzi wa NHC inayoendelea katika Hoteli ya Tanga Beach Resort.
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora, Erasto Chilambo akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Isikizya zilizopo wilayani Uyui mkoani Tabora kwenye semina ya mameneja na wakurugenzi wa NHC inayoendelea katika Hoteli ya Tanga Beach Resort.
Washiriki wa Semina hiyo Wenceslaus Tillya, Meneja wa NHC mkoa wa Temeke, Nehemia Msigwa, Meneja wa NHC Katavi na Daniel Nkya wakifuatilia kwa kina somo lililokuwa likitolewa na Wataalamu Washauri wa Delloite Touche juu ya mapitio ya Mpango Mkakati wa Shirika unaomalizika mwakani, ili kuuboresha kwa kipindi kijacho. Somo hilo lilitolewa kabla ya mawasilisho ya mameneja wa mikoa.
Meneja Mshauri Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte Bw.Frederick Nsemwa, Mkurugenzi wa Watushi Housing Limited, Dk Fred Nsemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakifuatilia somo hilo.
Wataalamu washauri wa semina hiyo wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu, James Rhombo na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki Benedict Kilimba wakifuatilia semina hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni