.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Desemba 2014

AJALI YA LORI LA SHABA NYORORO IRINGA, MAGARI YAKWAMA KUENDELEA NA SAFARI

Watumiaji wa barabara ya Iringa Njombe wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261 BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita.

Mtandao huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya njombe Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama kwenye msururu huo.

Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa. Baadhi ya abiria na madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia ufinyu vya kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo muda mrefu(karibia siku moja).

Hali hiyo iliondolewa majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo yakaendelea na safari. ( Kwa hisani ya Edwin Moshi wa Eddy Blog)

               Tayari barabara imefunga, magari hayawezi kupita foleni ni kubwa
                                      Barabara imefunga pande zote mbili hakuna pa kupita
                           Msusuru wa magari kama unavyoonekana kufuatia ajali hiyo








Jitihada za kulitoa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni