.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 27 Januari 2015

RAIS KIKWETE AMTEUA GODFREY MNGEREZA KUWA KATIBU MTENDAJI BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kuwatangazia Wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amemteua ndugu Godfrey Lebejo Mngereza kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Barua ya Januari 16, 2015 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga imeeleza kwamba uteuzi wa Mngereza unaanza Januari 23, 2015.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Mngereza alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kwa kipindi cha kutoka Februari 2013 hadi 2015 mwanzoni akitokea Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii ya BASATA aliyokuwa akiiongoza kama Mkurugenzi wake.

Godfrey Mngereza ni msomi mwenye shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amepata kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu hicho katika Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) hadi mwaka 2008 alipoajiriwa rasmi na BASATA kama Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari ambayo kwa sasa inafahamika kama Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii.

Aidha, shahada yake ya kwanza ilikuwa katika masuala ya Sanaa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Imetolewa na Kitengo cha Habari- BASATA

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni