Serikali imesema kuwa
ipo tayari, kuongeza muda wa kuandikisha watu katika daftari la
kudumu la wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa BVR, iwapo Tume ya
Uchaguzi (NEC) itakabiliana na matatizo wakati wa uandikishaji na
kuiomba serikali kufanya hivyo.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo
Pinda ametoa kauli hiyo leo wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi
ya upinzani bungeni, Mhe. Freeman Mbowe aliyehoji, uwezo wa
kuandikisha wapigakura milioni 24, kwa muda uliowekwa wakati mashine
za BVR zinauwezo wa kuandikisha watu 22 tu kwa siku.
Mhe. Pinda amesema taarifa alizonazo
kutoka kwa Tume ya Uchaguzi ni kuwa awali mashine hizo zilikuwa na
uwezo wa kuandikisha watu 74 kwa siku, lakini baada ya kufanyiwa
majaribio tume ya uchaguzi ilibaini kuwa zinauwezo wa kuandikisha
mara mbili ya idadi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni