.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Machi 2015

MAGAIDI WALA NJAMA YA KUFANYA SHAMBULIO KWENYE BUNGE LA KENYA

Magaidi wapatao 12 inaaminika kuwa wanapanga kufanya shambulio katika bunge la Kenya, vyanzo vya polisi vimetahadharisha, na kupelekea majengo yote ya serikali kuwekwa katika hali ya tahadhari.

Taarifa za Kiintelejensia zinaeleza kuwa miongoni mwa magaidi hao, sita kati yao inawezekana tayari wapo Jijini Nairobi, na wengine sita hawajajulikana walipo.

Taarifa za uwezekano wa kuwepo shambulio hilo, zimekuja wakati ubalozi wa Misri Jijini Nairobi kuviomba vyombo vya dola Kenya kuimarisha ulinzi katika majengo ya Misri pamoja na Ubalozi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni