Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akipokea
Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Switzerland
hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, leo Tarehe 25-08-2015
ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri Bernard Membe
akizungumza na Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe.
Florence Tinguely Mattli, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yakiendelea huku Msaidizi
wa Waziri Bw. Thobias Makoba (kulia) akisikiliza na kufuatilia
mazungumzo hayo na Afisa wa Mambo ya Nje Bi. Olivia Maboko (kushoto)
naye akifuatilia mazungumzo hayo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akiagana
na Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe.
Florence Tinguely Mattli, leo Tarehe 25-08-2015 ofisini kwake jijini
Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwasilisha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni