Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amesema ushindi wa timu yake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza
hapo jana utawaudhi wengi kwa kuwa watu hupenda kuona mabingwa
wakipoteza mechi.
Katika mchezo huo beki wa Chelsea
John Terry alitolewa nje kwa kadi nyekundu hata hivyo walifanikiwa
kushinda kwa mabao 3-2 dhidi ya West Brom.
Hata hivyo Pedro alikuwa na mwanzo
mzuri baada ya kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza tu tangu
anunuliwe kutoka Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 21.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni