.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 24 Agosti 2015

KOCHA RAFA BENITEZ AMEANZA KIBARUA CHA KUINOA REAL MADRID KWA SARE TASA

Kocha Rafa Benitez ameanza kibarua cha kuinoa Real Madrid kwa kutofanya vyema katika La Liga baada ya timu yake kulazimishwa sare tasa na timu iliyopanda daraja ya Sporting Gijon.

Real Madrid ikiwa imefunga magoli 11 katika michezo nane ya kujiandaa na msimu, imejikuta ikiachia pointi mbili muhimuna kuwa nyuma ya Barcelona na Atletico Madrid baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza ya mechi za La Liga.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha Banitez nchini Hispania tangu miaka 11 kupita alipoondoka Valencia kwenda Uingereza kuinoa Liverpool.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni