.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 25 Agosti 2015

MASHA APANDISHWA KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU

Aliyewahikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Laurence Masha, leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka.

Akiwa mbele ya Hakimu Waliyarwande Lema, Masha amesomewa shtaka la kutoa lugha ya matusi kwa Afande Juma Mashaka jana jioni katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini Dar es Salaam alipoenda kuwawekea dhamana vijana 17 wa kundi maarufu la linalojulikana kwa jina la Kingereza kama 4U Movement.

Mshtakiwa Masha alikana shtaka hilo, na kupewa sharti la dhamana ya shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili, lakini alishindwa kutimiza masharti ya dhamana kutokana na muda wakazi kuishi na kurejeshwa rumande, kesi yake itasikilizwa tena tarehe 7 mwezi ujao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni