.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 25 Agosti 2015

NSSF, NEEC ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO LEO JIJINI DAR ES SALAAM



MKURUGENZI wa Shirika Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau amewataka madereva na wamiliki wa pikipiki za Bodaboda kuwa na utamaduni wa kurudisha mikopo wanayopata kupitia Zao ili iweze kuzungushwa kwa bodaboda wengine.


Dau ametoa rai hiyo leo wakati alipokuwa akitia saini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati NSSF na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).
“Hamkufanya makosa kujiunga Saccos, kwa kuwa nina imani mtapata nafasi ya kukopeshwa na mtapata maendeleo, hivyo ni matarajio yangu kuona kwamba yule bodaboda aliyepata mkopo siku moja nije kusikia anamiliki ndege,” alisema Dau.
Makubaliano hayo ya mkopo wenye thamani ya Shilingi bilioni moja yalitiwa saini na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa, huku akishuhudiwa na wanachama wa Chama Cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Cha Wendesha Bodaboda Jijini Dar es Salaam.
Mkataba huo uliotiwa saini jana una lengo la kuisaidia serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwasaidia vijana kutambua fursa na nafasi yao katika maendeo ya taifa, kama sehemu ya jitihada za kuchangia katika kukabiliana na tatizo la kuzalisha mali kwa ajili ua ujenzi wa uchumi.

“Mkataba tunao saini leo ni moja ya jitihada za kuchangia katika kukabiliana na tatizo hili. Kuanzishwa kwa programu hii kutasaidia vijana katika sekta hii ndogo ya usafirishaji kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kununua pikipiki zao wenyewe, kuanzisha au kuendeleza biashara nyingine na pia kupata huduma za matibabu na huduma nyingine zilizotolewa na NSSF,” alisema.
Fedha za dhamana kwa ajili ya programu hiyo zitawekwa katika Benki ya Posta na NSSF itatumia fedha zake kukopesha vijana kwa ajili ya kununulia pikipiki kwa lengo la kufikia hesabu walizokubaliana na waajiri wao, matokeo yake kusababisha ajali mara kwa mara.
Akiweka wazi sifa na mashari ya wanachama ambao wataweza kukopesha ni wale ambao watakuwa wako kwenye vyama kuweka na kukopa, Saccos ambavyo vimesajiliwa kisheria.



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni