Maandamano ya siku ya tatu
yanaandaliwa nchini Lebanon ambapo watu wanaoipinga serikali wamekuwa
wakipambana na polisi kutokana na kushindwa kuondolewa taka kwenye
mitaa.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Tammam
Salam ametishia kujiuzulu wakati maelfu ya watu wakiandamana katika
Jiji la Beirut siku ya jumapili.
Polisi wamelazimika kutumia maji ya
kuwasha pamoja na mabomu ya machozi kuwasambaza watu na makumi ya
watu wamejeruhiwa. Lebanon haina rais na bunge lake nalo limekwama.
Polisi wakipambana na waandamanaji Lebanon
Marundo ya takataka ambazo hazijazolewa chini ya barabara ya juu



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni