.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 4 Agosti 2015

WATU WANNE WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAMEUWAWA NA POLISI

Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wameuwawa katika majibishano Makali ya risasi na Jeshi la Polisi katika eneo la Chapwa lililopo nje kidogo ya mji wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea wakati Majambazi hao walipo jaribu kumteka wakala wa kampuni ya TBL Thadeo Sanga na kumpora kiasi cha shilingi laki mbili ,gari aina ya Suzuki V6 T215 BLZ Pamoja na Bastola yake yenye numba 815859.

Wakizungumza na kituo hiki wameeleza kuwa baada ya uporaji huo majambazi hao walifanikiwa kutoweka eneo la tukio kwa kutumia gari la wakala huyo ambalo hata hivyo baadaye liliwashinda na Kupinduka.

Aidha wakiwa katika hali ya sintofahamu majambazi hao walitelekeza gari na kukimbilia porini ili kujiokoa huku wakifwatiliwa na wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Majambazi hao ambao hata hivyo hawakutambulika majina na Makazi waliko toka walikutwa na Bunduki mbilia aina ya SMG na Steering Gun ambazo zilikuwa zinatumiwa na majambazi hao kwa uporaji.

Miili ya marehemu hao ambao wameuwawa kwa ujmbazi imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Momba ikisubili utambuzi wa ndugu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni