.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 14 Februari 2016

DANNY WELBECK AREJEA KWA KISHINDO WAKATI ARSENAL IKIIZAMISHA LEICESTER CITY KWA MABAO 2-1

Timu ya Arsenal imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza timu ya Leicester City katika mchezo ambao wageni Foxes walimaliza wakiwa na wachezaji 10 katika dimba la Emirates.

Leicester City walipata bao lao kupitia kwa mshambuliaji wao nyota Jamie Vardy ambaye alipewa penati yenye utata na yeye kutofanya ajizi na kuutumbukiza kimiani mpira huo wa adhabu.

Danny Simpson alilambwa kadi nyekundu baada ya kuwa tayari na kadi ya njano ya kwanza kwa kucheza rafu, huku Theo Walcott aliyetokea benchi akiisawazishia Arsenal zikiwa zimebakia dakika 20 mpira kuisha naye Danny Welbeck aliyerejea uwanjani akitokea kwenye majeruhi akifunga mpira wa kichwa dakika za nyongeza na kuipa Arsenal ushindi.
          Jamie Vardy akishangilia goli la penati na wachezaji wenzake wa Leicester City
                     Danny Simpson akishika kichwa asiamini kadi nyekundu aliyopewa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni