Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya
(ICC) leo itatoa uamuzi wa rufaa iliyofunguliwa na Naibu Rais wa
Kenya, William Ruto, rufaa ambayo itatoa msimamo wa kesi inayomkabili
katika mahakama hiyo.
Majaji wa rufaa wa mahakama hiyo ya
ICC, wataamua kama ushahidi uliorekodiwa siku za nyuma usiwasilishwe
katika kesi inayowakabili Ruto na mwandishi wa habari Joshua Sang.
Rekodi zinaonyesha kwanini mwendesha
mashtaka Fatou Bensouda, anataka ushahidi huo ubakie mahakamani, na
kwanini mawakili wa washtakiwa wanataka ushahidi huo uliorekodiwa
kuondolewa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni