ZOEZI kusaka nyota wapya (vijana) ambao wataingizwa kwenye timu
mbili za Mbeya City Fc U20 na ile ya wakubwa limefikia kwenye hatua
nzuri hivi sasa baada ya wachezaji 44 kupatikana kwenye mchujo wa awali
alifanyika kwa siku nne mfululizo.
Akizungumza na mbeyacityfc.com, mara baada ya kumalizika kwa mazoezi
ya leo (Clinic day 5) kwenye uwanja wa Sokoine kocha msaidizi wa City,
Mohamed Kijuso amesema kuwa Vijana 44 wamefanikiwa kuvuka kwenye mchujo
wa kwanza hivyo wataingia kwenye wamu ya pili inayotaraji kuanza hapo
kesho kwenye uwanja wa Sokoine.
“Tulikuwa na kundi kubwa la wachezaji zaidi ya 106, baada
ya mchujo leo, tumefanikiwa kupata 44 ambao wataingia kwenye awamu ya
pili hapo kesho, lengo letu ni kuona tunapata Cream nzuri kwa ajili ya
timu yetu ya vijana na pia wachezaji saba ambao watakuwa tayari kucheza
kwenye timu kubwa msimu ujao”, alisema.
Kuhusu lini itakuwa siku ya mwisho, kocha huyo kijana alitanabaisha
kuwa, mchakato huu wa kuska vipaji ulikuwa ufikie tamati hapo kesho
lakini uongozi wa City umeamua kusogeza mbele mpaka siku ya jumamosi
ambapo wachezaji watakaopatikana kwenye mchujo wa kesho watapata
nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Ilemi Fc.
“Ilikuwa tuhitimishe kesho lakini tumesogeza mpaka
jumamosi ambapo vijana wetu wapya watakaopatikana watacheza mchezo wa
kirafiki , na baada ya hapo zoezi litafungwa tayari wa kusubiri
maandalizi ya msimu mapema mwezi ujao” alimaliza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni