Kiongozi wa zamani wa Chad, Hissene
Habre, ametiwa hatiani kwa uhalifu dhidi ya binadamu na amehukumiwa
kifungo cha maisha katika kesi ya kihistoria nchini Senegal.
Jaji wa Mahakama wamemtia hatiani
kwa ubakaji, utumwa wa ngono na kuagiza muaji wakati wa utawala wake
kuanzia mwaka 1982 hadi 1990.
Familia za waathirika wa matendo
hayo ya kikatili na mauaji wameshangilia na kukumbatiana mahakamani
baada ya hukumu hiyo kutolewa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni