.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Juni 2016

FASTJET YATANGAZA SHINDANO LINGINE KWA WATEJA WAKE

 Fastjet, shirika la ndege la bei nafuu Afrika limezifanya ndoto za usafiri kuwa za kweli kwa abiria wake zaidi ya milioni mbili waliopaa anga za Afrika tangu kuzinduliwa kwake Novemba 2012.

Ukiwa kama mkakati wa kuhamasisha hata Watanzania wengi zaidi kusafiri, fastjet imetangaza kwamba abiria yeyote anayenunua tiketi kuanzia Jumanne Mei 31 ataingia kwenye bahati na nasibu ya kwanza ya aina yake ijulikanayo Big 10 draw ambapo washindi 10 watasafiri bure katika njia yoyote ya fastjet katika mtandao wake barani Afrika.

Kwa watu kumi watakaoshinda bahati nasibu hiyo shirika linawapa uwezo wa kwenda katika mapumziko au kwenda katika safari ya manunuzi pamoja na marafiki na familia jambo wamekuwa wakiliwazia kila mara.

Ama kwa wajasiriamali wa Tanzania, safari hiyo inaweza kutumia kukuza mahitaji ya biashara kwa kuokoa gharama za usafiri katika safari nyingine kumi wanazozihitaji kusafiri.
 

“Ni rahisi, lengo la fastjet ni kufanya uwezekano kwa wateja wengi kusafiri, iwe ni kwa shughuli za biashara, kutembelea marafiki na familia, au kufurahia burudani ya kusafiri,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania John Corse.

Njia ambazo zinahusiana kwa ajili hiyo ni safari za kutoka Dare es Salaam kwenda Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Nairobi, Entebbe, Lusaka, Harare na Johannesburg hali kadhalika safari kati ya Kilimanjaro na Harare.
 

Tiketi zitakazonunuliwa Jumanne Mei 31, 20016 kwa njia za kimataifa na za ndani zitawawezesha abiria wake kuingia katika bahati nasibu ya Big 10. Washindi watatangazwa Juni 2016 na safari 10 za bure ni lazima zifanyike kabla ya Desemba 11, 2016.

Ikitambuliwa kama shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, fastjet hivi sasa inafanya safari ndani ya nchi 11 kwa wafanyabiashara, watali na familia ambazo zimeipokea tozo lake la nauli nafuu na linalofikia kwa usafiri wa anga.
 

“Usafiri wa anga ni ufunguo unaoendelea kuhamasisha na kukuza uchumi wa Tanzania kwa kuufanya uwe rahisi kwa familia, wafanya biashara na watalii kumudu kusafiri,” alisema Corse na kuongeza, “tumezindua punguzo hili la nauli hivyo kwamba hata wasafiri wanaweza kuzoea usafiri wa anga wanaoumudu, iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au mapumziko.”

Kukata tiketi kiunaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia www.fastjet.com, kupitia wakala aliyethibitishwa au kwa kuwasiliana na na fastjet kupitia +255 784 108 900. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu, kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi au malipo kwa njia ya mitandao ya simu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni