.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 24 Machi 2017

KAMPUNI YA MAHINDRA KUISAIDIA ZANZIBAR KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa ili kutoka Kushoto akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mji wa New Delhi Nchini India kwenye Makamo Makuu wa Shirikisho la Viwanda Mjini New Delhi.
Wa kwanza kutoka Kulia ni Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kampuni ya
Mahindra Bwana Arvind Mathew, wa kwanza kutoka Kushoto ni Mjumbe wa
Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mamboya na Kushoto ya Balozi Seif
ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mh. Mihayo Juma
N’hunga.
Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kampuni ya Mahindra Bwana Arvind Mathew Kushoto akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Balozi Seif akizungumza katika kikao cha pamoja mkati ya Ujumbe wake na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Mji wa New Delhi na Majimbo jirani yanayouzunguuka Mji huo makamo Makuu ya Shirikisho la Viwanda la India Mjini New Delhi. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila na Kulia yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bibi Asha Ali Abdulla.
Balozi Seif akimzawadia mlango Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila mara baada ya kumaliza mazungumzo
yao

Picha na – OMPR – ZNZ.


Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi katika utengenezaji wa vyombo vya
Moto ya Mahindra yenye Makao Makuu yake Mjini New Delhi Nchini India
imeamua kuiunga Mkono Zanzibar katika muelekeo wake wa kuimarisha
miradi ya maendelelo.

Mkuu wa shughuli za Kimataifa wa Kampuni hiyo Bwana Arvind Mathew
alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa
Kampuni yake na Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kilichofanyika Makao Makuu ya
Kampuni hiyo yaliyopo Mjini New Delhi.
Bwana Arvind Mathew alisema kutokana na kukuwa kwa Teknolojia ndani
ya Kamupuni ya Mahindra, Uongozi wa Taasisi hiyo ya Uhandisi Nchini
India hivi sasa umekusudia kuelekeza nguvu zake katika Mataifa rafiki
kwa nia thabiti ya kuona Mataifa hayo hasa yale ya Bara la Afrika
yanakuwa Kiuchumi.
Alisema Mahindra imejipanga kuangalia njia za kusaidia uimarishaji wa
Sekta ya Kilimo kupitia miundombinu imara na vifaa vya Kisasa
vitakavyoongeza nguvu za uzalishaji kwa kundi kubwa la Wakulima katika
mazao ya viungo yenye tija kubwa katika soko la Kitaifa na Kimataifa.
Alisema Wataalamu wa Kampuni ya Mahindra wamekuwa shahidi katika
safari zao za kawaida kwenye Mataifa mbali mbali waliyowekeza miradi
yao ya Kiuchumi kuwaona Wakulima wa maeneo hayo wakiendesha shughuli
zao katika mazingira magumu.
Bwana Arvind Mathew alieleza kwamba wakulima wengi hasa katika Nchi
changa zinazojikita kuendelea wamekosa Taaluma ya kutosha katika
kuimarisha Kilimo chao jambo ambalo wanadiriki kupata kipato kidogo
huku wakitumia nguvu nyingi zaidi wakati wa uzalishaji.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara cha Kampuni ya Mahindra Kanda ya Afrika Bwana Saurabh Kohli aliueleza Ujumbe wa Zanzibar ulio
mwishoni mwa ziara yake Nchini India kwamba Mahindra imekusudia kuwa
na Mtandao wa Kimataifa katika mfumo wa Uzalishaji katika Nchi mbali
mbali walizowekeza Ulimwenguni.
 
Bwana Saurabh Kohli alisema Mahindra iliyoasisiwa kwama 1945 ikianza
na uzalishaji wa gari aina ya Jeep kwa sasa tayari imeshawekeza katika
Mataifa Mia Moja kwenye nchi mbali mbali Duniani ikiwa na wafanyakazi
wasiopungua Laki 200,000 ikianza na mtaji wa Dola za Kimarekani U$
Bilioni 16.5.
 
Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe wake Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Seif alisema ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Zanzibar
na Kampuni ya Mahindra umetoa mchango mkubwa katika kuwakomboa
Wananchi na hasa Wakulima wa Zanzibar.
 
Alisema Wananhi wa Zanzibar zaidi ya asilimia 70 walioko Vijijini
katika Visiwa vya Unguja na Pemba wanaendesha maisha yao ya kila siku
kwa kutegemea sekta ya Kilimo.
 
Wakati huo huo Ujumbe wa Zanzibar ulikutana kwa mazungumzo na
Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara tofauti wa Mji wa New Delhi na
Majimbo jirani yanayouzunguuka Mji huo yaliyofanyika Makamo Makuu ya
Shirikisho la Viwanda la India { CII }.
 
Katika mazungumao yao Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo
ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K
Kapila alisema India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla zimekuwa
na ushirikiano wa karibu wa Kibiashara uliotiwa saini mnamo mwaka
1974.
 
Bwana Kapila alisema ushirikikano huo unaoendelea kuimarika kila siku
umeibuwa mchango mkubwa wa msaada wa fedha zitakazosaidia uimarishaji
wa huduma za Maji safi na salama katika Mkoa wa Mjini Magharibi
Zanzibar kufuatia ziara ya mwaka jana ya Uongozi wa ngazi ya juu ya
India uliofika Tanzania Mwezi Disemba mwaka 2015.
 
“ Uwepo wa wafanyakazi zaidi ya 10,000 wanaotoka Nchini India
wakifanya kazi Tanzania na Zanzibar kwa ujumla ni uthibitisho wa
ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili.
 
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alisema Zanzibar imeshafungua milango ya uwekezaji kwa makampuni mbali
mbali ndani na nje ya Nchini tokea miaka ya 90.
 
Alisema zipo sekta ambazo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeshazijengea uwezo kwenye miundombinu itakayotoa wepesi kwa Taasisi
pamoja na Makampuni yenye nia na maamuzi ya kutaka kuwekeza miradi
yao ya Kiuchumi Visiwani Zanziobar.
 
Balozi Seif aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa inapatikana katika
sekta ya Afya, Kilimo, Miundombinu, Elimu pamoja na sekta isiyo ya
kiserikali inayotoa ajira kubwa zaidi kwa makundi ya akina mama na
Vijana.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni