.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 24 Machi 2017

KIUNGO WA TOTTENHAM DELE ALLI AFUNGIWA MECHI TATU ULAYA

Kiungo wa Tottenham, Dele Alli, amefungiwa kucheza michezo mitatu ya michuano ya Ulaya baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi ya Uropa dhidi ya Gent.

Alli alitolewa nje kwa kadi mwezi Februari baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Gent, Brecht Dejaegere, katika mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2.

Iwapo Tottenham itamaliza kwa kushika nafasi tatu za juu katika Ligi Kuu ya Ungereza, Alli atakosa nusu ya kampeni za michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
                                          Dele Alli akimchezea rafu mbaya mchezaji Dejaegere

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni