.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 20 Machi 2017

KONGAMANO LA MAADILI KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano la maadili litakalofanyika kesho Uwanja wa Taifa kuanzia saa nne asubuhi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza. Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inatarajia kufanya kongamano linalolenga maadili kwa Taifa nchini.Kongamano hilo litafanyika kesho kuanzia saa nne asubuhi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema ni wajibu kwa kila mwanajamii kuthamini, kuenzi na kuendeleza maadili mema, mila na desturi zinazofaa.

“Serikali hususani wizara inajukumu la kutoa muelekeo na usimamizi kuhakikisha Taifa linaenzi na kuimarisha utambulisho wake na kujenga utamaduni huru na sio huria” alisemaWambura.

Aidha Wambura alisema kuna fursa ya kubaini, kuenzi na kukuza, kuhifadhi na kurithisha utamaduni na sanaa vyenye kuzingatia na kuimarisha maadili, mila na desturi kwa kuleta maendeleo.

“Wananchi wamekuwa wanaendelea kujihusisha na shughuli mbalimbali za Kifani, Sanaa na utamaduni ikiwemo ngoma za asili, filamu, muziki, jando, unyago, matambiko, Sherehe na maadhimisho mbalimbali” alisemaWambura.

Ameongeza kuwa shughuli hizo ni halali ilimradi zifanywe kwa kuzingatia sheria na kanuni na msingi wa asili yake, kwa maana kwamba kama jambo ni la faragha na usiri libaki kwenye uhalisia wake na kuhusisha rika jinsia na asili yake.

( Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni