.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Mei 2017

ARSENAL YAKOSA NAFASI YA KUTINGA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Arsenal imekosa nafasi ya kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20, licha ya kuifunga Everton kwa magoli 3-1.

Kikosi cha kocha Arsene Wenger kilipata ushindi wanaostahili licha ya beki Laurent Koscielny kutolewa nje kwa kucheza rafu ya kizembe.

Arsenal walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Hector Bellerin na kisha kuongeza la pili kupitia kwa Alexis Sanchez na latatu la Ramsey. Romelu Lukaku alifunga kwa penati.
Kocha Arsene Wenger akiwa ameinamisha kichwa chini baada ya kuikosa nafasi ya nne Ligi Kuu ya Uingereza
Hata hivyo Liverpool ilihakikisha haikosi nafasi ya nne baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Middlesbrough na kufanikiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akishangilia kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya nne Ligi Kuu ya Uingereza

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni