.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 17 Mei 2017

ARSENAL YAZIDI KUWEKA PRESHA MBIO ZA KUMALIZA NNE BORA LIGI KUU YA UINGEREZA

Arsenal inahakikisha mbio za kuwania kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Uingereza zinaamuliwa hadi dakika ya mwisho baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Sunderland.

Katika mchezo huo wa jana Alexis Sanchez alifunga goli la kwanza akiunganisha pasi ya Mesut Ozil katika dakika ya 72 na kuamsha hamasa katika dimba la Emirates.

Goli hilo liliamsha hamasa kwa Arsenal na  kulishambulia goli la Sunderland na alikuwa Sanchez tena aliyefunga goli la pili akinasa mpira uliopigwa na Olivier Giroud.
                                 Alexis Sanchez akifunga goli lake la kwanza katika mchezo huo
         Alexis Sanchez akitumbukiza goli la pili akinasa mpira uliopigwa na Giroud

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni