.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Mei 2017

BALOZI SEIF AHUTUBIA JUKWAA LA UCHUMI WA DUNIA MJINI AMMAN, JORDAN

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika Warsha ya Sekta ya Utalii ndani ya Jukwaa la Uchumi wa Dunia {World Economy Forum} Mjini Amman Jordan alipokuwa akiwasilisha muelekeao wa Tanzania katika kuimarisha Utalii na fursa zinazopatikana kwa Taasisi zinazotaka kuwekeza miradi yao Tanzania.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa miongoni mwa Viongozi walioshiriki Jukwaa la Uchumi la Dunia ambao wa kwanza kutoka kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mastacard Bibi Tara Nathan akibadilishana mawazo na Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia Mjini Amma Jordan.
Balozi Seif akibadilishana Mawazo na Waziri wa Mambo ya Nchi za nje wa Jordan Bwana Iman Safad mara baada ya ufunguzi wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Mjini Amma Nchini Jordan.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kiwa pamoja na Viongozi wenzake wa Kimataifa walioshiriki ufunguzi wa Jukwaa la Dunia la Uchumi {WEF} Nchini Jordan.
Balozi Seif Kati kati katika picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasilisha muelekeao wa Tanzania katika kuimarisha Utalii na fursa zinazopatikana kwa Taasisi zinazotaka kuwekeza miradi yao Tanzania kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia Mjini Amma Jordan.
 

                                                                                                   Picha na – OMPR – ZNZ.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni