.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Mei 2017

BALOZI SEIF AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MTENDAJI MKUU WA MFUKO WA MAENDELEO WA MFALME ABDULLA WA PILI WA JORDAN

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi kati kati akisailiana n a Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa
Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus kwenye Hoteli
ya Kimataifa ya Kemisk Mjini Amman Nchini Jordan.

Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Baishar, Viwanda na Masoko Z
anzibar Balozi Amina Salum Ali.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme
Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus akizungumza na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mjini Amma Nchini Jordan.
Bwana Rami Al – Qusus Kushoto akisisitiza jambo
wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Kempisk Nchini Jordan.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar
Balozi Amina Salum Ali wa Pili kutoka Kulia akifafanua jambo wakati
Ujumbe wa Viongozi wa Tanzania ulipofanya mazungumzo na Ujumbe wa
Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan.

Kushoto yaBalozi Amina ni Balozi wa Tanzania Ukanda wa Mashariki ya
Kati Balozi Mohamed Haji Hamza, kulia ya Balozi Amina ni Balozi Seif
Ali Iddi, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa
Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus pamoja na Mjumbe wa Bodi ya
wadhamini ya Mafuko huo Bwana Haitham Hammour

Balolzi Seif kati kati akiwa katika picha ya
pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Mfuko wa Mfalme Abdulla wa Pili wa
Jordan na ule wake uliotoka Tanzania kushiriki Jukwaa la Dunia la
Uchumi Nchini Jordan.

Kulia ya Balozi Seif ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme
Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al – Qusus pamoja na Mjumbe wa
Bodi ya wadhamini ya Mafuko huo Bwana Haitham Hammouri.

Kushoto ya Balozi Seif ni:- Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Zanzibar Balozi Amina Salum, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Balozi wa Tanzania
Ukanda wa Mashariki ya Kati Balozi Mohamed Haji Hamza.
Balozi Seif Kulia akiagana na Mtendaji Mkuu wa
Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan Bwana Rami Al –
Qusus na anayeshuhudia wa kwanza kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya
wadhamini ya Mafuko huo Bwana Haitham Hammouri.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameushauri na
kuuomba Uongozi wa Mfuko wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan kufikiria
namna unavyoweza kusaidia Taaluma na hata uwezeshaji mifuko ya
Tanzania ili iweze kufanikiwa vyema kiutendaji kama ulivyopiga hatua
kubwa ya maendeleo Mfuko huo.
Balozi Seif alitoa ushauri na ombi hilo wakati akizungumza na Mtendaji
Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan hapo
katika moja ya Kumbi za Mikutano ya Hoteli ya Kimataifa ya Kempisk
Mjini Amman akiwa Nchini humo kushiriki Jukwaa la Dunia la Uchumi
akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe
Magufuli.
Alisema mifuko mingi iliyoanzishwa Nchini Tanzania imekuwa ikikabiliwa
na ufinyu wa Taaluma na hata nguvu za kifedha zinazoweza kuiendesha
kwa umakini zaidi hali ambayo baadhi yake ikishindwa kufanyakazi na
kudumaa kabisa kiutendaji.
 
Balozi Seif alisema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi tofauti
zikiwemo zile za Kiraia na hata za Mataifa ya kigeni zimekuwa zikitoa
muongozo wa namna ya Jamii inavyoweza kuendesha miradi yao kwa
kujikimu Kimaisha na kupunguza ukali wa Maisha ikisaidiwa na Mifuko
iliyopo lakini bado nguvu za kujitegemea kwa Jamii hiyo zinaonekana
kusua sua.
 
Aliualika Uongozi huo wa Mfuko wa Mafalme Abdulla wa Pili wa Jordan
kufika Tanzania kujionea Mifuko iliyopo jambo ambalo kwa mtazamo huo
wanaweza kuata picha halisi na ikiwezekana Taaluma na maarifa
uliyonayo watendaji wake unaweza kuona jinsi gani unaweza kusaidia.
 
Balozi Seif alisema ipo mifuko ya Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF
}, Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi iliyoanzishwa kwa lengo mahsusi la
kusaidia Jamii kupambana na ukali wa maisha lakini bado Jamii ya
wananchi walio wengi wanaendelea kukabiliwa na maisha duni kutokana na
ufinyu wa Bajeti ya Mifuko hiyo isiyoweza kukidhi mahitaji ya Watu
wote.
 
Alieleza kwamba Serikali zote mbili zilizopo Tanzania ile ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa na
mipango mbali mbali iliyoanzishwa kama Mifuko ya kujitegemea ili
kusaidia Wananchi hasa Vijana kuweza kupata njia zitakazowasaidia
kujiendesha Kimaisha.
 
Alisema njia hizo ni mbadala badala ya kusubiri kutegemea ajira za
Taasisi za Umma ambazo kwa sasa zimepunguwa kwa kiasi kikubwa kutokana
na kukua kwa Teknolojia ya kisasa inayotoa fursa kwa fanyakazi
wachache kuwajibika kwa kutumia mfumo huo.
 
Naye Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum
Ali alisema licha ya Mfuko wa Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan kutoa
huduma kwa Wananchi wa ndani ya Jordan pekee lakini bado una nafasi ya
kuangalia jinsi unavyoweza kusaidia Tanzania katika misingi ya
kudumisha ushirikiano na uhusiano ulipo kati na Mataifa hayo mawili.
 
Balozi Amina alisema uhusiano wa Kihistoria unaoendelea kuunganisha
Jordan na Tanzania unaweza pia ukatumika kusaidia uanzishaji wa
miradi ya pamoja itakayoweza kustawisha zaidi Wananchi wa pande hizo
mbili rafiki.
 
Mapema Mtendaji Kuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Mfalme Abdulla wa Pili wa
Jordan Bwana Rami Al – Qusus aliueleza Ujumbe wa Tanzania kwamba Mfuko
huo uliasisiwa na kupewa nguvu za kiuwezeshaji kutoka kwa Kiongozi
huyo ili usaidie Jamii katika mipango wanayojipangia ya Maendeleo.
 
Bwana Al – Qusus alisema Mfuko huo ambao kwa sasa unajitegemea wenyewe
bila ya kupata msaada au ruzuku kutoka sehemu nyengine yoyote
unaendelea kutoa Mikopo, kusaidia miradi inayoanzishwa na Vijana,
Maendeleo ya Uchumi, Kilimo pamoja na Utalii.
 
Alisema misaada hiyo inakwenda sambamba na ile ya ustawi wa jamii kwa
kuwajengea uwezo zaidi Wanawake ambao ndio wahimili wakubwa
wanaotegemewa na familia na Taifa mahali popote pale.
 
Mtendaji Kuu huyo wa Mfuko wa Maendeleo ya Mfalme Abdulla wa Pili wa
Jordan alifahamisha kwamba katika mbinu za kuujengea uwezo zaidi wa
kiutendaji Mfuko huo, Uongozi wake umeshafungua Matawi yasiyopungua 13
katika maeneo mbali mbali ya Jordan ikiwemo pia Saudi Arabia na Oman.

Aliuhakikishia Ujumbe wa Tanzania kwamba Jordan kupitia Mfuko huo wa
Maendeleo wa Mfalme Abdulla wa Pili bado una nafasi ya kushirikiana na
Tanzania katika uanzishwaji wa miradi ya maendeleo inayoweza kusaidia
Jamii ya pande zote mbili rafiki.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/5/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni