.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 17 Mei 2017

BALOZI SEIFA AENDA JORDAN KUHUDHURIA JUKWAA LA UCHUMI LA DUNIA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akiagana na Mjumbe wa Baraza la Mainduzi ambae pia ni Waziri
asiye na Wizara Maalum Mh. Said Soud Said kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Abeid Aman Karume akiondoka kupitia Dar es salaam kwa
safari ya kuhudhuria Tamasha la Uchumi la Dunia { World Economy }
linalotarajiwa kufanyika Amman Nchini Jordan.
Balozi Seif akiagana na Viongozi mbali wa Serikali
na Taasisi za Umma kuelekea Nchini Jordan kwenye kumuakilisha Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufili kwenye
Tamasha hilo la siku Tatu linaloanza Tarehe 19 Mei 2017
Balozi Seif akisalimiana na Wahudumu wa Ndege ya
Tropical akijiandaa kuanda kupitia Mjini Dar es salaam kwa safari ya
Mjini Amman Nchini Jordan akiambatana na Waziri wa Biashara, Viwanda
na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.


Picha na – OMPR – ZNZ.

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka
Zanzibar kupitia Mjini Dar es salaamu kuelekea Amman Nchini Jordan
kuhudhuria Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Forum - WCF} la
Siku Tatu litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58
Duniani.
Balozi Seif  anamuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya
Kati na Kaskazini mwa Afrika litakaloshirikisha Vingozi Wakuu wa Nchi,
Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, Wawakilishi wa
Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja na
Vijana.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar
Balozi Seif  Ali Iddi aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi
ameagwa na Mwaziri, baadhi ya Watendaji Wakuu  wa Serikali pamoja na
Viongozi wa Kisiasa.
Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif
ameongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar  Balozi
Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.


Tarehe 19 Mei Balozi Seif na Ujumbe wake atashiriki Washa ya Utalii
itakayojikita zaidi katika masuala ya Kujenga Uchumi kwa Mataifa ya
Mashariki ya Kati na yale ya Kanda ya Afrika  ili kuona njia gani
zinaweza kutoa fursa za ajira kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya
Kisasa Warsha  itakayofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Kempisk
Mjini Amman Jordan.
Jukwaa hilo la Uchumi Duniani litafunguliwa na Kiongozi wa Jordan
Mfalme wa Pili Abdullah  Bin Al-Hussein asubuhi ya Tarehe 20 Mei
kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa King Hussein Bin Talal katika Bahari
Nyeusi.
Baadawe Waziri wake anayehusika na Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa
akiwa pia Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdullah Bwana
Imad Fakhoury atapata wasaa wa kuwasilisha  mpango wa maendeleo wa
Taifa hilo.
Mpango huo umekuja kufuatia  mabadiliko makubwa ya uchumi yaliyofanywa
na Nchi hiyo ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita  pamoja na
kutafuta mbinu ya kupata utulivu na Amani wa Mashariki ya Kati na
Kanda ya Afrika  kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi lililosababishwa
na vita kwenye maeneo hayo.
 
Jordan imekuwa  muandaaji maarufu wa Jukwaa la Dunia la Uchumi { World
Economy Forum }kwa takriban mara Tisa sasa na 16 kwa Kanda na
Mashariki ya Kati ya Kaskazini mwa Afrika ambapo Viongozi wa Mataifa
ya palestina, Misri, Kosovo, Iraq, Tanzania  na Morocco wanatazamiwa
kushiriki Jukwaa hilo.
Mabadiliko makubwa ya uchumi yaliyofanywa na Jordan ndani ya kipindi
cha miaka kumi iliyopita yameliwezesha Taifa hilo la kiarabu kufungua
milango ya Uwekezaji katika sekta za Nishati, Usafiri, Mipango ya
Maendeleo ya Miji, huduma za Maji safi, Miundombinu ya Mawasiliano,
Utalii pamoja na Mtandao wa Mawasiliano wa Kompyuta { ICT }.
Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum - WCF} limeasisiwa
Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake  Profesa Klaus
Schwab huko Davos, Switzerland.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa 9ili wa Rais wa Zanzibar
17/5/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni