.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 24 Mei 2017

BOMU LA KUTEGWA ARIDHINI LAUWA POLISI WATATU NCHINI KENYA

Polisi watatu nchini Kenya wameuwawa leo asubuhi na wengine wawili wamejeruhiwa wakati gari lao lilipokanyaga bomu la kutengenezwa kienyeji katika eneo la Liboi, kaunti ya Garissa.

Maafisa wengine watatu wamenusurika katika tukio hilo lililotokea katika majira ya saa kumi na mbili alfajiri.

Polisi wamesema gari hilo ni la kituo cha polisi Kulan, ambalo lilikuwa linaelekea Liboi wakati lilipogonga gonga bomu lililotegwa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab la nchini Somalia.
                Gari la polisi likiwa limeharibika baada ya kukanyaga bomu lililolipuka

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni