.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 28 Mei 2017

BONDIA KELL BROOK ADUNDWA NA ERROL SPENCE JR

Bondia Kell Brook amedundwa na Errol Spence Jr na kupoteza ubingwa wa dunia wa IBF uzito wa welterweight.

Brook, ambaye alikuwa amefanyiwa upasuaji katika jicho lake la kulia miezi nane iliyopita, alikuwa hajapona vyema na lilivimba mno kati kati ya pambano lao.

Bondia huyo mkazi wa Sheffield aliangushwa chini katika raundi ya 10 kwa makonde makali ya Spence Jr lakini alinyanyuka na kuendelea na pambano.

Hata hivyo aliweza kumudu raundi iliyofuata kabla ya refa Howard Foster kumaliza pambano licha ya Brook kunyanyuka baada ya kuhesabiwa hadi kudikia tisa. 
                                                 Bondia Errol Spence Jr akimpiga ngumi Kell Brook
            Bondia Errol Spence Jr akishangilia baada ya kumpeleka chini Kell Brook

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni