.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 28 Mei 2017

CHALES MWIJAGE AFUNGUA MAONYESHO YA TANO YA BIASHARA TANGA

Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako Tanga. Mwijage ameyafungua maonyesho hayo leo katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa jana Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.

Waziri wa viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa pamoja na mafuta aina mbalimbali.


Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho Tanga

Wakazi wa Tanga wakiangalia Kobe ambaye ni moja ya vivutio katika maonyesho ya tano ya Kimataifa yanayofanyika Tanga. blog ya kijamii ya tangakumekuchablog 0655 902929

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni