.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Mei 2017

CHELSEA WAKABIDHIWA KOMBE LAO WAKIMALIZA LIGI KWA USHINDI

Timu ya Chelsea imekabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu ya Uingereza huku ikimaliza ligi kwa ushindi mnono wa magoli 5-1 dhidi ya timu ya Sunderland inayoshuka daraja, katika mchezo ambao pia kapteni John Terry aliagwa rasmi.

Katika mchezo huo Chelsea walijikuta wakifungwa goli la mapema na Javier Manguillo lakini walizinduka haraka na kusawazisha kupitia kwa Mbrazil Willian, kabla ya baadaye Eden Hazard kuongeza la pili.

Pedro aliyeingia kuchukua nafasi ya Hazard alifunga goli tatu kupitia kosa la mpira wa kichwa wa kurudishwa nyuma uliopigwa na Joleon Lescott huku mchezaji mwingine aliyetokea benchi Michy Batshuayi kufunga magoli mawili.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte alijikuta akimwagiwa maji ikiwa ni sehemu ya furaha ya ushindi
Kocha Muitaliano Antonio Conte akibusu kombe la Ligi Kuu ya Uingereza waliolitwaa
Mshambuliaji nyota Diego Costa  ambaye hatma yake ya kubakia Chelsea ipo mashakana akiwa akiwa amebeba kombe
Nohodha John Terry aliyestaafu soka rasmi akitoa shukurani na neno lake la mwisho kwa mashabiki baada ya kuichezea Chelsea kwa miaka 22

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni