.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Mei 2017

KIPA SERGIO ROMERO AIPA MANCHESTER UNITED SARE DHIDI YA SOUTHAMPTON

Kipa Sergio Romero ameokoa kiufundi michomo kadhaa wakati Southampton na Manchester United wakitoka sare katika dimba la St Mary's.

Southampton walikuwa waongoze katika dakika ya tano wakati Eric Bailly kumkamata mchezaji katika eneo la penati, lakini kipa United, Romero akaokoa penati ya Manolo Gabbiadini.

Shoti kali la Bailly nalo liliokolewa na kipa Fraser Forster, baada ya beki huyo kutengeneza nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Southampton walimpa kazi ya ziada kipa Romero ya kuokoa mashuti yao, huku naye Anthony Martial akiachia shuti la umbali wa yadi 25 lililogonga mwamba.
Manolo Gabbiadini akipiga mpira wa penati huku wachezaji wenzake wakiufuatilia kwa kuuangalia
Kipa wa Manchester United Sergio Romero akiufuata mpira wa penati uliopigwa na kuupangua

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni