.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 29 Mei 2017

MASHINDANO YA COPA UMISSETA YAZINDULIWA JIJINI DAR

Mchezaji wa Shule ya Sekondary Chang’ombe, Hamad Hemed (kulia), akiwania mpira na mchezaji wa Shule ya Makongo, Muksin Mohamed, wakati wa michuano ya Copa/UMISSETA yaliodhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola, kwenye Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam
Mchezaji wa Shule ya Sekondari Makongo (kushoto), akiwania mpira na mchezaji wa Shule ya Chang’ombe Tarik Hassan, wakati wa michuano ya Copa/UMISSETA yaliodhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akikagua timu za Sekondary zilizoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA Dar es Salam mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa timu za Sekondari zilizoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA Dar es Salam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa kampuni ya Coca-Cola Bw. Eric Ongara akiongea machache wakati wa ufunguzi wa michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akifungua michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akigawa vifaa vya michezo kwa shule za sekondari zinazoshiriki michezo ya Copa/UMISSETA.

Dhana ya kuwekeza katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari imekua ikileta manufaa makubwa kwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao wamekua wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya chini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akifungua michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

“Nimefurahishwa na juhudi zinazofanywa na kampuni ya Coca-Cola katika kuhakikisha tunaimarisha sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa kupata wanamichezo mahiri wa baadaye” amesema Waziri Mwakyembe.

Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja na kuchangia katika uchumi wa nchi. Vilevile aliwataka walimu kufuata ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha michezo mashuleni ikiwemo kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio kuvitumia vipindi hivyo kwa shughuli nyingine.

Mhe. Mwakyembe aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanawapatia watoto wao nafasi ya kucheza na kujifunza michezo mbalimbali inayowajenga kimwili na kiakili.“Michezo inafaida kubwa kwa afya ya binadamu ikiwemo kuimarisha akili na mwili, kujenga ushirikiano na urafiki baina ya watu “ alisema Mhe. Mwakyembe.

Naye Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa kampuni ya Coca-Cola Bw. Eric Ongara alisema kuwa kampuni ya Coca-Cola inaamini katika kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini ndio maana wamekua wakidhamini mashindano hayo.

Pia aliongeza kuwa kampuni ya Coca-Cola itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa michezo inazaa matunda na kufikia lengo lililokusudiwa la kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza.

Michezo ya COPA UMISSETA ilifunguliwa rasmi Mjini Dodoma Aprili 28 mwaka huu ambapo kitaifa yanatarajiwa kuanza Juni 6 hadi 15 mwaka huu katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni