.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Mei 2017

MSICHANA AKATA NYETI ZA KIONGOZI WA KIROHO INDIA KWA MADAI YA KUMBAKA

Msichana wa miaka 23 nchini India amemkata sehemu za siri kiongozi wa kiroho wa Kihindu katika jimbo la kusini la Kerala, kwa madai kuwa alikuwa akimbaka kwa miaka mingi.

Polisi wamesema mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Gangeshananda Theerthapada, alikuwa akienda kwenye nyumba ya msichana huyo kufanya matambiko kwa ajili ya afya ya baba yake.

Mama wa msichana huyo alikuwa na matumaini kuwa kiongozi huyo wa kiroho atasaidia kutakasa mikosi inayoiandama familia yake, lakini sasa mtoto wake amedai alikuwa akimbaka kila mara.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni