.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Mei 2017

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG ATWAA TUZO YA MFUNGAJI BORA UJERUMANI

Mshambuliaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ameifungia Borussia Dortmund goli la mkwaju wa penati la dakika za mwisho katika siku ya mwisho ya msimu wa Ligi ya Bundesliga na kuwa mfungaji anayeongoza kwa kufunga magoli 31.

Katika mchezo huo wa jana Aubameyang alifunga magoli mawili wakati Dortmund ikiifunga Werder Bremen 4-3, goli lake la kwanza akilipata dakika tatu kabla ya mapumziko na la pili katika dakika ya 89.

Aubameyang anakuwa mchezaji wa pili kutoka Afrika kutwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu nchini Ujerumani, baada ya Mghana Tony Yeboah kutwaa tuzo hiyo mara mbili wakati akiichezea timu ya Eintracht Frankfurt katika msimu ya 1992-93 na 1993-94.
                            Pierre-Emerick Aubameyang akibusu tuzo yake ya ufungaji bora 
   Pierre-Emerick Aubameyang akipongezwa na wachezaji wenzake kwa kutwaa tuzo hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni