.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 24 Mei 2017

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA KAMATI MAALUM YA KWANZA ILIYOFANYA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI ULIOTAKIWA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI KUTOKA KWENYE MACHIMBO YA MADINI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingalia Taarifa hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakwanza kulia wakishuhudia tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigusia baadhi ya mambo yaliyomo kwenye Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakisikiliza wakati mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Uchunguzi wa Mchanga wa Madini Profesa Abdulkarim Hamis Mruma alipokuwa akiiwasilisha.
Baadhi ya Mawaziri pamoja na Wabunge wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya Kamati
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kupokea Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.

Wasanii mbalimbali wa Nyimbo za Bongo Flavour na Dansi wakiimba wimbo wa Amani Tanzania kabla ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Wasanii mbalimbali wa Nyimbo za Bongo Flavour na Dansi walipokuwa wakiimba wimbo wa Amani Tanzania kabla ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini nchini.
Viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa nao wakifatilia Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma akisoma dondoo za Ripoti aliyoikabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya uchunguzi wa Mchanga wenye madini Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa mchanga wenye Madini Profesa Abdulkarim Hamis Mruma pamoja na Wajumbe wa Kamati Hiyo mara baadaya kupokea Taarifa ya Uchunguzi huo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni