.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Mei 2017

RONALDO AVUNJA REKODI NYINGINE WAKATI REAL IKIFUKUZIA UBINGWA WA LA LIGA

Cristiano Ronaldo amevunja rekodi aliyoweka Jimmy Greaves miaka 46 ya rekodi ya kufunga Ulaya wakati Real Madrid ikisogea na kubakisha pointi moja tu kuweza kutwaa ubingwa wa La Liga tangu mwaka 2012.

Ronaldo aliifungia Real Madrid goli la kwanza na kufanya kufikia magoli 367 katika ligi tano za juu za Ulaya, na kufikia rekodi iliyowekwa na mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Greaves mwaka 1971.

Ronaldo akafunga tena goli la pili baada ya John Guidetti kuipamatumaini Celta iliyokuwa na wachezaji 10 kwa kufunga goli, huku mshambuliaji Mfaransa Karim Benzema na Toni Kroos wakifunga nao goli moja kila mmoja.

Real Madrid watatangazwa kuwa mabingwa wa La Liga jumamosi iwapo watatoa sare tu na Malaga ambayo ipo katika nafasi za kati katika msimamo wa ligi.
                                      Cristiano Ronaldo akijipinda na kuachia shuti lililozaa goli 
                               Mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo ukiwa umejaa wavuni

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni