.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 26 Mei 2017

SERIKALI ZA TANZANIA NA UGANDA ZATILIANA SAINI MKATABA WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda
Ujumbe wa Tanzania na Uganda ukishuhudia tukio la utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi, akihutubia baada ya kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Bw. George Masaju (kulia) na Mwanasheria wa Uganda Bw. Milliam Byaruhanga (kushoto), wakionesha nakala za Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakionesha Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, baada ya kuusaini, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
 

                                                                (Picha na Wizara ya Fedha na Mipango)

                                                                                                     Na Benny Mwaipaja, WFM

Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania lenye urefu wa Kilometa 1,443, uliokadiriwa kugharimu zaidi ya Dola bilioni 3 nukta 55, mjini Kampala Uganda, leo.

Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi na Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Marais wa Nchi hizo mbili, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Hafla ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo yatapitishwa katika bomba hilo hilo.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni