.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Mei 2017

TAREHE RASMI YA KUANZA KWA MKUTANO WA KIMATAIFA WA OYES 2017 YAJULIKANA.

Tarehe rasmi ya kuanza kwa mkutano mkubwa wa kitaifa na kimataifa wa OYES (Open your Eyes and See) 2017 unaoandaliwa kila mwaka na kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza imejulikana.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, amebainisha kwamba mkutano huo utaanza jumamosi Mei 27 na kufikia tamati jumapili Juni 04, 2017 katika viunga vya kanisa hilo vilivyopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza.

Kupitia BMG Habari, Dkt.Kulola amebainisha kwamba waimbaji na watumishi wa Mungu kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Mchungaji Gary White kutoka Amerika watahudumu katika mkutano huo.

Mafundisho pamoja na mahubiri ya neno la Mungu yaliyolenga kumfungua kila mmoja ili aone Ukuu wa Mungu yatafundishwa katika mkutano huo na kama ilivyo kawaida mamia ya wananchi wanatarajiwa kufunguliwa kwenye mkutano wa OYES 2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni