.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Mei 2017

TIMU YA MONACO YASHINDA UBINGWA WA LIGI 1 NCHINI UFARANSA

Timu ya Monaco imeshinda Ubingwa wa Ligi 1 kwa mara ya kwanza tangu miaka 17 kupita, baada ya jana kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Saint-Etienne.

Ikiwa inahitaji pointi moja tu kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo ya Ufaransa kwa mara ya nane, mchezaji aliyekatika kiwango bora kinda Kylian Mbappe alifunga goli la kwanza kiufundi.

Mbappe, 18, aliufuata mpira uliopigwa na kapteni Radamel Falcao na kudokoa juu ya kipa na kisha kuutumbukiza kimiani.

Mshambuliaji Valere Germain aliihakikishia ushindi Monaco kwa kufunga goli la pili katika dakika za mwisho.
                          Kinda Kylian Mbappe akifanya vitu vyake katika mchezo wa jana
               Wachezaji wa Monaco wakifurahia kutwaa kombe la ubingwa wa Ligi 1

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni