.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 17 Mei 2017

VIONGOZI WA KIJIJI CHA KIBADA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA KIJIJI KUONGOZA WANANCHI

Kushoto ni Jamali Juma afisa mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa vitendo (LEAT) akifuatiwa na Afisa habari wa LEAT Edina Tibaijuka pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili wakati wa mkutamo wa hadhara wa kijiji cha kibada ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha kibada
Hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa hadhara wenye lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na Maliasili za kijiji
Na Fredy Mgunda, Iringa.

Ili kuongoza au kusimamia jamii ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuondoa migogoro mbalimbali inajitokeza na itakayo kujitokeza kwa sababu ya kuzivunja sheria na taratibu hizo.
 
Hayo yamesemwa na Afisa mradi wa Mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira Jamali Juma wakati wa mkutano wa kijiji cha kibada kilichopo kata ya sadani wilayani Mufindi Mkoani Iringa kwa kuwataka viongozi na wananchi kutimiza wajibu na haki ili kukifanya kijiji kiwe na maendeleo.
Juma alisema kuwa sheria na taratibu zilizopo hapa kijiji zitanatakiwa kufuatwa kwa ajili ya manufaa ya sasa na ya kizazi kichacho lakini pia inajenga imani na amani ya kijiji.
 
"Leo hii usipofuata sheria na taratibu za kijiji lakina utakwazana na viongozi au wananchi na kupelekea migogoro ndani ya kijiji kwa kuwa sheria zinakuwa zimekiukwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977" alisema Juma
 
Aidha Juma aliwataka viongozi wa kijiji cha kibada kuitisha mikutano ya hadhara na kuwasomea mapato na matumizi ili wananchi wajue wapi kijiji kimetoka kimaendeleo na ipi mikakati ya kimaendeleo kijiji.
 
"Ukipita vijiji vingi unakuta migogoro mingi inayotokana na kutosomewa mapato na matumizi kwa sababu binafsi za viongozi husika hivyo ni lazima viongozi wa vijiji kuongoza vijiji kwa kufuata sheria na taratibu za kijiji"alisema Juma
 
Lakini Juma aliwataka wananchi wa kijiji cha kibada kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na Maliasili walizonazo na kuacha kuishi kwa mazoea ili kuboresha Mazingira ili yarudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia.
 
"Jamani kuna njia nyingi za kulima mboga mboga kwa njia ya kisasa kwa mfano unaweza kuchukua gunia au sarufeti na kuuweka mchanga kisha kupanda mbegu za mboga na kumwagilia maji machafu unayokuwa unayatumia nyumbani kwao na kuvifanya vyanzo vya maji kuwa salama" alisema Juma
 
Fadinard yilikwipande,Shauri na Stephano waliitaka serikali kuanga upya sheria za kilimo cha mboga mboga kilinacholimwa kwenye utongo mnyevumnye au karibu na vyanzo vya maji kwa akili ya kilimo changu kwa ajili ya kujiongezea kipato chao.
 
"Sisi tunalima kwenye vijaruba vidogo vidogo tu maarufu kama vinyungu wala hatuleti madhara yoyote ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mbona miaka yote tulikuwa tunalima bila kuharibu Mazingira na serikali itambue kuwa Kilimo hiki ni cha kitamaduni sasa inatakiwa kutofautisha sheria za mambo ya asili au ya kitammaduni"walisema wananchi wa kibada
 
Kwa upande wake Afisa habari wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za Mazingira kwa vitendo (LEAT) Edina Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kuzifuata sheria walizoletewa za kulinda Mazingira na vyanzo vya maji hadi pale serikali itakapoa tamko liingine kuhusu hiyo sheria.
 
"Jamani sheria ni msumeno hivyo mnapaswa kuzifuata kwa kuwa msipozifuta mtatiwa nguvuni na kupelekwa mahakama hivyo itakuwa inawapunguzia nguvu kazi yenu na kupelekea Msumbufu kwa familia zenu,Mimi nawaomba tiini sheria bila shuruti ili kuepukana na hayo matatizo" alisema Tibaijuka
 
Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kupelekea malalamiko yao kwa viongozi wa serikali, madiwani na wabunge wao ili kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo la sheria hiyo mpya iliyokuja baada makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu la kukataza Kilimo chochote kile kwenye vyanzo vya maji.
 
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili aliwaomba viongozi wa serikali kuifikiria upya sheria waliyoitunga juu ya matumizi ya vyanzo vya maji kwa kuangalia utamaduni wa watu Vijijini hasa kwenye swala la Kilimo cha kipindi cha kiangazi maeneo ya mabondeni kwa kuwa wananchi wa Vijijini wantegemea kilimo hicho.
 
"Hivi kama huku wilaya ya Mufindi wakulima wanategemea Kilimo cha kulima kwenye mabonde maarufu kama Kilimo cha kwenye vinyungu kwa kupanda mboga mboga pamoja na mahindi ya msimu wa kiangazi"alisema Nyavili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni