.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Mei 2017

WATU 140 WAMEKUFA KATIKA SHAMBULIZI LA KAMBI YA UWANJA WA NDEGE LIBYA

Ripoti zinaeleza kuwa watu wengi wapatao 140, wakiwemo raia wamekufa katika shambulizi kwenye kambi ya uwanja wa ndege wa jeshi nchini Libya.

Awali ilizaniwa kuwa watu 60 walikufa wakati wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali walipokuwa wakijaribu kutwaa kambi hiyo ya Brak al-Shati siku ya Alhamisi.

Waziri wa Ulinzi wa Libya wa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa pamoja na kamanda wa wapiganaji wote wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Waziri Mkuu wa Libya amekanusha kutoa amri ya kufanyika kwa shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu wengi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni