Mshambuliaji wa Manchester City
Gabriel Jesus amekosa goli la wazi kabla ya baadaye kuondolewa akiwa
amebebwa kwenye machela wakati Brazil ikifungwa goli moja kwa bila na
Argentina Mjini Melbourne.
Katika mchezo huo wa kirafiki
Argentina ilipata goli pekee kupitia kwa shambulizi lililofanywa na
Gabriel Mercardo na kumpatia kocha Jorge Sampaoli mwanzo mzuri wa
kuiongoza timu hiyo.
Jesus alipoteza nafasi nzuri ya
kusawazisha katika kipindi cha pili wakati alipomzunguka kipa Sergio
Romero lakini shuti lake liligonga mwamba na kutoka nje kabla ya
kutolewa nje katika dakika za mwisho za mchezo baada ya kugongwa
usoni.
Beki wa Sevilla Gabriel Mercardo akishangilia goli alilofunga
Gabriel Jesus akiwa amemzunguka kipa Romero lakini akashindwa kufunga
Gabriel Jesus akiwa amebebwa kwenye machela baada ya kuumia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni