.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 6 Juni 2017

BALOZI SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA TMF

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na kubadilishana mawazo na Uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { TMF } hapo Ofisini kwake kwenye Majengo ya Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Media Foundation Nd. Ernest Sungura.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Media Foundation Nd. Ernest Sungura kushoto akimueleza Balozi Seif Mikakati ya TMF katika kuwafinyanga Wanahabari kuandika Habari na Makala yaliyofanyia Utafiti na Uchunguzi.
Ujumbe wa Viongozi wa TMF uliofanya mazungumzo na Balozi Seif wa kwanza kushoto ni Mwanakhamis Mparu Mwenyekiti wa Bodi ya Redio Iqra na Bibi Florah Boniface Magabe Mshauri wa Waandishi wa Habari wa TMF.
Balozi Seif Ali Idi Kati kati akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania uliofika Ofisini kwake majengo ya Baraza la Wawakilishi kubadilishana mawazo.
Balozi Seif akiagana na Uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania uliofika Ofisini kwake majengo ya Baraza la Wawakilishi kwa mazungumzo.


Picha na – OMPR – ZNZ.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura amesema hadhi ya Sekta ya Habari Nchini itaheshimika na kuaminika zaidi endapo wanahabari wenyewe watajiwekea malengo ya kufanya kazi kwa agenda katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Alisema mfumo wa agenda kwa Wanahabari ndio njia pekee itakayosaidia kuamsha ari sambamba na kuibua changamoto zinazokwaza Jamii na kuzipa nguvu za uwajibikaji Taasisi za Umma na hata zile binafsi katika kuwahudumia kwa umakini Wananchi.

Nd. Ernest Sungura Alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa TMF uliokuwepo Zanzibar kwa ziara maalum ya kukagua Maandalizi na Mikakati ya mradi wa kuwapatia Mafunzo Wanahabari wa Zanzibar.

Alisema kupitia Mfuko wa Vyombo vya Habari zipo agenda zilizowahi kuibuliwa na Wanahabari wa Vyombo tofauti Nchini akizitolea mfano Escro, Dawa za Kulevya, Udhalilishaji wa Kijinsia na Ubalozi wa Usalama Bara barani ambazo zimesaidia kuleta faraja kwa Jamii na kuzipunguzia matumizi mabovu yasiyo na msingi Serikali zote mbili.

Alieleza kwamba yapo mambo mengi na mazuri ya kujivunia kutokana na kuanzishwa kwa mfumo huo wa agenda jambo ambalo limeziletea sifa Taasisi za Habari kwa Taifa na Wananchi jambo ambalo lilisaidia kuibua changamoto zinazokwaza Serikali na Jamii kwa ujumla.

Bwana Sungura alimueleza Balozi Seif kwamba katika kuwajengea uwezo uliobobea Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa kazi zao TMF mwaka huu imeshatenga Fedha Maalum kwa ajili ya kuwapatia mafunzo Wanahabari wasiopungua Mia 600 kutoka vyombo 120 vya Habari Nchini.

Alisema mkazo zaidi wa mafunzo hayo utawekwa kwa wale waandishi na Vyombo vya Habari visivyo na uwezo wa kufanyakazi vizuri ili navyo viweze kupiga hatua itakayokwenda sambamba na wenzao wenye nguvu za uwezeshaji kifedha.

Naye Mshauri wa Waandishi wa Habari wa TMF Bibi Florah Boniface Magabe alisema Zanzibar inaweza kupiga hatua kubwa zaidi kiuchumi kama itaamua kuzitangaza fursa za Utalii zilizopo Visiwani Unguja na Pemba.

Bibi Florah alisema michezo ya Utalii wa Uzamiaji inayopendwa sana na Watalii Duniani inaweza kufungua njia pana zaidi ya ongezeko la idadi ya watalii wanaoingia Zanzibar na kuikaribia Nchi ya Misri inayokusanya mapato makubwa kupitia fani hiyo ya michezo ya Baharini.

Alipendekeza utangazi huo wa Utalii wa Uzamiaji unaweza kutumiwa katika Matamasha mbali mbali yanayoandaliwa Zanzibar likiwemo lile la Sauti za Bisara, ZIFF pamoja na Tamasha la Mzanzibari yanayokusanya wageni wengi kutoka Mataifa mbali mbali Duniani.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { TMF } kwa uamuzi wake wa kuwafinyanga Wanahabari katika misingi ya kuwajibika Kitaaluma zaidi badala ya kukurupuka katika Uandishi wao.

Balozi Seif alisema kitendo cha Taasisi hiyo cha kuwajengea uwezo wa Kitaaluma Wana Tasnia hao wa Habari kitawawezesha kuzalisha zao litakalopokewa vyema tena kwa Heshima kutoka kwa Jamii.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar5/6/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni