.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Juni 2017

BALOZI SEIF AONGOZA MAZIKO YA MWANASIASA MKONGWE VISIWANI ZANZIBAR, MZEE KHAMIS MKADARA

Mwanasiasa Mkongwe wa Zanzibar Mzee Khamis Mkadara aliyefariki Dunia
mapemba leo asubuhi amezikwa Kijijini kwake Wawi Mkoa wa Kusini Pemba
maziko yaliyohudhuriwa na Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu, Wananchi pamoja na Viongozi wa Kiserikali na Kisiasa.


Mzee Khamis Mkadara alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya kawaida pamoja
na uzee alifariki nyumbani kwake Mtaa wa Wawi Wilaya ya Chake chake
Mkoa wa Kusini Pemba.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika mazishi
hayo aliiwakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Chama
cha Mapinduzi akijumuika na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr.
Juma Abdulla Mabodi na baadhi ya watendaji wa Serikali.


Marehemu Mzee Khamis Juma Mkadara alizaliwa Mwaka 1927 na kuanza elimu ya Quran katika Madrasa mbali mbali za Wilaya ya Chake chake ambapo
baadaye katika ujana wake akajishughulisha na masuala ya Kisiasa
katika dhana nzima ya kudai Uhuru wa Visiwa vya Zanzibar.


Katika kipindi hicho ya kutaka kujikomboa Mzee Mkadara alikuwa
muanzilishi wa Chama cha Shirazy Association na baadaye kukiunganisha
na chama cha African Association na Kuzaliwa kwa Chama cha Afro
Shirazy Party.


Katika utumishi wa Chama Mzee Khamis Juma Mkadara aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa ASP wa Wilaya ya Chake chake mwaka 1973 na baada ya
kuzaliwa Chama cha Mapinduzi mwaka 1977 aliendelea na wadhifa huo hadi
mwaka 1997.


Mbali ya wadhifa huo wa Kichama Mzee Mkadara pia aliwahi kuwa Diwani
wa Wadi ya Wawi mwaka 1995.


Mwanasiasa huyo mkongwe Kisiwani Pemba alikuwa mstawi wa mbele katika
utetezi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar akiwa miongoni mwa Wazee
waliotumikia kwa kiindi kirefu Taifa hili la Tanzania.


Utumishi huo uliweza kumpatia fifa na ushujaa uliopelekea kutunukiwa
nishani na Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Nne Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar wa Awamu ya Sita Dr. Aman Abeid
Karume.


Mzee Khamis Juma Mkadara aliyefikisha umri wa Miaka 90 ameacha Kizuka
Mmoja, Watoto Wanane na Wajukuu 33.


Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Mwanasiasa huyo Mkongwe Mzee Khamis
Juma Mkadara mahali pema peponi. Amin.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
7/6/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni